MENU

Where the world comes to study the Bible

Mpango wa Mungu wa Wokovu

Related Media

1 Yoh 5:11-12 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

Mkutadha huu watwambia ya kwamba Mungu ametupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe, Yesu Kristo. Katika maneno mengine, njia ya kuumiliki uzima wa milele ni kummiliki Mwana wa Mungu. Swahili ni, mtu awezaje kukuwa na Mwana wa Mungu?

Shida ya Mwanadamu

Utengano na Mungu

Isaya 59:2 Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso Wake msiuone, hata hataki kusikia maombi yenu.

Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Kulingana na Warumi 5:8, Mungu alionyesha pendo Lake kwetu sisi kwa njia ya mauti ya Mwanawe. Kwa nini ilimpasa Kristo kutufia? Kwa sababu Andiko la tangaza watu wote kuwa wafanya dhambi. Kufanya "dhambi" kuna maanisha kukosa alama. Biblia inatangaza "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu (utakatifu mkamilifu) wa Mungu" (Rum. 3:23). Katika maneno mengine, dhambi zetu zatufarikisha sisi na Mungu wetu aliye utakatifu mkamilifu (haki na kweli) na kwa hivyo sharti Mungu awahukumu watenda dhambi.

Habakuki 1:13a Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, Wewe usiyeweza kutazama ukaidi; mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya?

Matendo yetu Yasioleta Manufaa

Andiko lafundisha pia ya kwamba hakuna kiasi cha wema wa mwanadamu, matendo ya binadamu, tabia njema ya binadamu, au utendaji wa kidini uwezao kumfanya mtu akubalike na Mungu wala kumwingiza mtu mbinguni. Mtu wa kidini, na mtu mwovu na yule asiye wa kidini wote wako katika hali moja. Wote walipungukiwa na haki ya ukamilifu wa Mungu. Baada ya kujadili mtu mwovu, mtu mwadilifu, na mtu wa kidini katika Warumi 1:18-3:8, Mtume Paulo atangaza ya kwamba Wayahudi na Wayunani wote wako chini ya dhambi, ya kwamba "hakuna mwenye haki hata mmoja" (Rum. 3:9-10). Yaliyo ongezwa kwa jambo hili ni maazimio yafuatayo ya vifungu vya Maandiko:

Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu asije akajisifu.

Tito 3:5-7 alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema Yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema Yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.

Warumi 4:1-5 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? 2 Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; (lakini si mbele za Mungu). 3 Maana Maandiko yasemaje? "Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki." 4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini Yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

Hakuna kiasi cha wema wa binadamu ulio wema jinsi alivyo Mungu. Kwa sababu ya jambo hili, Habakuki 1:13 inatwambia Mungu hawezi kuwa na ushirika na mtu ye yote asiyekuwa na haki kamilifu. Ili tukaweze kukubalika na Mungu, sharti tuwe wema jinsi alivyo Mungu. Mbele za Mungu, sisi sote twasimama uchi, wasiojiweza, na wasio na tumaini ndani yetu. Hakuna kiasi cha kuishi kuzuri kitakacho tupeleka mbinguni wala kutupa uzima wa milele. Jawabu ni nini basi?

Utatuzi wa Mungu

Mungu si utakatifu mkamilifu tu (ambaye tabia Yake sisi hatuwezi kamwe kuifikilia kwa nafsi zetu wa kwa matendo yetu ya haki) lakini Yeye pia ni pendo kamilifu aliyejaa neema na huruma. Kwa sababu ya pendo Lake na neema, Yeye hajatuwacha sisi bila tumaini na jawabu.

Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, Tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Hii ni habari njema ya Biblia, ujumbe wa injili. Ni ujumbe wa kipawa cha Mwana wa Mungu Mwenyewe aliyefanyika mwanadamu (Mungu-mwanadamu), akaishi maisha yasiyo ya dhambi, akafa msalabani kwa ajili yetu, naye akafufuliwa kutoka kaburini akitoa jambo ya kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu na thamani ya mauti Yake kwa ajili yetu kama kibadala.

Warumi 1:4 aliyedhihirishwa kwa uwezo kuwa Mwana-wa-Mungu, kwa jinsi ya Roho Mtakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.

Warumi 4:25 Ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

2 Wakorintho 5:21 Mungu alimfanya Yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.

1 Petro 3:18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili Wake akauawa, bali roho Yake akahuishwa.

Je, Twampokeaje Mwana wa Mungu?

Kwa sababu ya kile alichotimiza Yesu Kristo kwa ajili yetu pale msalabani, Biblia inaeleza "Yeye aliye na Mwana anao uzima." Twaweza kumpokea Mwana, Yesu Kristo, kama Mwokozi wetu kwa imani ya kibinafsi, kwa kutumaini katika utu wa Kristo na katika mauti Yake kwa ajili ya dhambi zetu.

Yohana 1:12 Bali wote waliompokea--wale waliaminio jina Lake--aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.

Yohana 3:16-18 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaniniye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Hili linamaanisha sharti kila mmoja wetu aje kwa Mungu kwa njia ile hasa: (1) kama mtenda dhambi afahamuye dhambi zake, (2) aziye tambua ya kwamba matendo ya binadamu yanaweza kuleta wokovu, na (3) kuegemea juu ya Kristo peke Yake kabisa kwa imani peke kwa ajili ya wokovu wetu.

Ikiwa ungependa kumtumaini na kumpokea Kristo kama Mwokozi wako wa binafsi, huenda unataka kuieleza imani yako iliyo katika Kristo kwa ombi rahisi kwa kubali uovu wako, ukikubali msamaha Wake na kuiweka imani yako katika Kristo kwa ajili ya wokovu wako.

Ikiwa wewe umetumaini katika Kristo kwa muda usio mrefu, unahitaji kujifunza kuhusu maisha yako mapya na jinsi ya kuenenda pamoja na Bwana. Labda tuna pendekeza uanze kupitia kusoma zile ABCs for Christian Growth yapatikanayo kwa http://www.bible.org. Hizi mfululizo safu utachukua moja-kwa-moja kupitia baadhi ya kweli ya msingi wa Neno la Mungu na utakusaidia wewe kwa kujenga msingi imara kwa ajili ya imani yako katika Kristo.

Related Topics: Soteriology (Salvation)

Report Inappropriate Ad